Nembo ya TartilTartilRedio mubashara

Sura Az-Zalzalah: maandishi na tafsiri ya maana

Sura ya 99 katika Msahafu, aya 8, inaanzia ukurasa wa 599.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura Al-BayyinahSura Al-Aadiyat ›

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

1. Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!

2. Na itakapotoa ardhi mizigo yake!

3. Na mtu akasema: "Ina nini?"

4. Siku hiyo itahadithia habari zake.

5. Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!

6. Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!

7. Basi anayetenda chembe ya wema, atauona!

8. Na anayetenda chembe ya uovu, atauona!

Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)

Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura Al-BayyinahSura Al-Aadiyat ›