Nembo ya TartilTartilRedio mubashara

Sura Al-Aadiyat: maandishi na tafsiri ya maana

Sura ya 100 katika Msahafu, aya 11, inaanzia ukurasa wa 599.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura Az-ZalzalahSura Al-Qari'ah ›

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

1. Ninaapa kwa farasi waendao mbio wakipumua.

2. Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini.

3. Wakishambulia wakati wa asubuhi.

4. Huku wakitimua vumbi.

5. Na wakijitoma kati ya kundi.

6. Hakika mwanadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!

7. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!

8. Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!

9. Kwani hajui watakapofufuliwa waliomo makaburini?

10. Na yakakusanywa yaliyomo vifuani?

11. Hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na habari zao wote!

Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)

Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura Az-ZalzalahSura Al-Qari'ah ›