Sura ya 104 katika Msahafu, aya 9, inaanzia ukurasa wa 601.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Ole wake kila anayewakejeli watu kwa ishara na maneno.
2. Aliyekusanya mali na kuihesabu.
3. Anadhani ya kuwa mali yake itambakisha milele!
4. Hasha! Hakika atavurumishwa katika Hutwama.
5. Na ni nini kitakachokujulisha ni nini Hutwama?
6. Ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa.
7. Ambao unapanda nyoyoni.
8. Hakika huo utafungwa sawasawa nao wako ndani yake.
9. Kwenye nguzo zilizonyooshwa.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.