Sura ya 105 katika Msahafu, aya 5, inaanzia ukurasa wa 601.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya wale wenye tembo?
2. Kwani hakufanya vitimbi vyao kuharibika?
3. Na akawatumia ndege makundi kwa makundi.
4. Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni.
5. Akawafanya kama majani yaliyoliwa!
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.