Nembo ya TartilTartilRedio mubashara

Sura Al-Fatihah: maandishi na tafsiri ya maana

Sura ya 1 katika Msahafu, aya 7, inaanzia ukurasa wa 1.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsirSura Al-Baqarah ›

1. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

2. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.[1]

[1] Mola Mlezi ni yule anayewalea walimwengu wote. Nao walimwengu ni kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu.

3. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.[1]

[1] Katika misingi waliyokubaliana juu yake watangulizi wema wa umma huu na maimamu wake ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ana majina na sifa nzuri nzuri.

4. Mmiliki wa Siku ya Malipo.

5. Ni Wewe tu tunayeabudu, na ni Wewe tu tunayeomba msaada.

6. Tuongoe kwenye njia iliyonyooka.

7. Njia ya wale uliowaneemesha. Siyo ya wale waliokasirikiwa, wala waliopotea.

Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)

Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsirSura Al-Baqarah ›