Sura ya 85 katika Msahafu, aya 22, inaanzia ukurasa wa 590.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Ninaapa kwa mbingu yenye nyota kubwa kubwa!
2. Na kwa Siku iliyoahidiwa!
3. Na kwa shahidi na kinachoshuhudiwa!
4. Wameangamizwa watu wa makhandaki.
5. Yenye moto wenye kuni nyingi.
6. Walipokuwa wamekaa hapo.
7. Na wao ni mashahidi wa yale waliyokuwa wakiwafanyia Waumini.
8. Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa walikuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.
9. Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu.
10. Hakika waliowafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.
11. Hakika walioamini na wakatenda mema watapata Bustani za mbinguni zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
12. Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
13. Yeye ndiye anayeanzisha na ndiye anayerejesha tena.
14. Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi.
15. Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu.
16. Atendaye ayatakayo.
17. Je! Zimekufikia habari za Majeshi?
18. Ya Firauni na Thamudi?
19. Lakini waliokufuru wamo katika kukadhibisha.
20. Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazingira.
21. Bali hii ni Qur-ani tukufu.
22. Katika Ubao uliohifadhiwa.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.