Nembo ya TartilTartilRedio mubashara

Sura Al-Inshiqaq: maandishi na tafsiri ya maana

Sura ya 84 katika Msahafu, aya 25, inaanzia ukurasa wa 589.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura Al-MutaffifinSura Al-Buruj ›

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

1. Itakapochanika mbingu.

2. Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza.

3. Na ardhi itakapotanuliwa.

4. Na kuvitoa vilivyokuwa ndani yake, ikawa tupu.

5. Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza.

6. Ewe mtu! Hakika wewe unafanya matendo kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.

7. Ama atakayepewa daftari lake kwa mkono wa kulia.

8. Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi.

9. Na arudi kwa ahali zake na furaha.

10. Na ama atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake.

11. Basi huyo ataomba kuteketea.

12. Na ataingia Motoni.

13. Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.

14. Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.

15. Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona vyema!

16. Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapokuchwa.

17. Na kwa usiku na unavyovikusanya.

18. Na kwa mwezi unapopevuka.

19. Lazima mtapanda tabaka kwa tabaka!

20. Basi wana nini hawaamini?

21. Na wanaposomewa Qur-ani hawasujudu?

22. Bali waliokufuru wanakanusha tu.

23. Na Mwenyezi Mungu anajua wanayoyadhamiria.

24. Basi wabashirie adhabu chungu!

25. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usiomalizika.

Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)

Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura Al-MutaffifinSura Al-Buruj ›