Sura ya 86 katika Msahafu, aya 17, inaanzia ukurasa wa 591.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Ninaapa kwa mbingu na kinachokuja usiku!
2. Na nini kitakachokujulisha ni nini hicho kinachokuja usiku?
3. Ni Nyota yenye mwanga mkali.
4. Hapana nafsi ila inaye mwangalizi.
5. Hebu na ajitazame mwanadamu ameumbwa kwa kitu gani?
6. Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa.
7. Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
8. Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
9. Siku zitakapodhihirishwa siri.
10. Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
11. Ninaapa kwa mbingu yenye marejeo!
12. Na kwa ardhi inayopasuka!
13. Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
14. Wala si mzaha.
15. Hakika wao wanapanga mpango.
16. Na Mimi napanga mpango.
17. Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.