Sura ya 114 katika Msahafu, aya 6, inaanzia ukurasa wa 604.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa watu.
2. Mfalme wa watu.
3. Mungu wa watu.
4. Kutokana na uovu wa Shetani mtia wasiwasi, ajifichaye mno (Al-Khannaas).
5. Anayetia wasiwasi katika vifua vya watu.
6. Kutokana na majini na watu.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.