Nembo ya TartilTartilRedio mubashara

Sura Al-Alaq: maandishi na tafsiri ya maana

Sura ya 96 katika Msahafu, aya 19, inaanzia ukurasa wa 597.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura At-TinSura Al-Qadr ›

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

1. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba.

2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu.

3. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!

4. Ambaye amefundisha kwa kalamu.

5. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui.

6. Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri.

7. Akijiona katajirika.

8. Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.

9. Umemuona yule anayemkataza.

10. Mja anaposali?

11. Umeona kama yeye yuko juu ya uongofu?

12. Au anaamrisha ucha Mungu?

13. Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?

14. Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?

15. Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!

16. Shungi la uongo, lenye makosa!

17. Basi na awaite wenzake!

18. Nasi tutawaita Mazabania!

19. Hasha! Usimtii! Nawe sujudu na ujongee!

Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)

Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura At-TinSura Al-Qadr ›