Sura ya 108 katika Msahafu, aya 3, inaanzia ukurasa wa 602.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Hakika tumekupa Al-Kawthar (heri nyingi).
2. Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.
3. Hakika anayekuchukia ndiye aliye mpungufu mno.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.